Monday, May 11, 2015

FILIKUNJOMBE akabidhi msaada wa shilingi milioni 40


Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe
MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe asema baadhi ya wabunge, mawaziri na watendaji wabovu serikalini wanakichafua chama cha mapinduzi (CCM).


Filikunjombe alisema kuwa CCM ni chama makini na kinachopendwa sana ila shida ipo kwa baadhi ya watu waliopo ndani ya CCM na serikali ni bomu.

Mbunge huyo alitoa kauli hiyo leo katika kijiji cha Mavanga wakati akijibu maswali ya wananchi na viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kuhusiana na CCM kuwateulia wananchi viongozi wasio na sifa kugombea nafasi mbali mbali.

Alisema kama kila mmoja angetimiza wajibu wake katika nafasi yake hakuna mpinzani ambae angechaguliwa ila kuchaguliwa kwa wapinzani ni kushindwa kwa wale waliowaamini kutoka Ccm kushindwa kuwajibika kwa wananchi waliowaamini

Filikunjombe alisema atakuwa mbunge wa mwisho kunyoshewa kidole na watanzania wakiwemo wananchi wake wa Ludewa kwa kushindwa kuwatumikia wananchi na chama chake cha Ccm .

Kwani alisema hakuomba ubunge kwa ajili ya kujinufaisha binafsi ila aliamua kugombea ili kuwatumikia wana Ludewa kwa kuwapelekea maendeleo hivyo kazi yake kwa sasa hadi mwisho wa ubunge wake ni kuleta maendeleo kwa wananchi wake na kuona ahadi zake zinatimia kwa muda uliopangwa na si kujinufaisha kwa wakati.

" Naomba kwanza mtambue kuwa wabunge wote tulipo fika bungeni kwa mara ya kwanza tulikopeshwa Tsh milioni 90 kwa ajili ya kununua gari la kutembelea na Mimi kwa kuwa nilikuwa na gari pesa hizo niliamua kununua gari la wagonjwa Mlangali ambao hawakuwa na gari la wagonjwa ....lengo langu kutumikia wananchi na kuwatatulia kero zao si vinginevyo"

Akielezea msaada huo wa vitu mbali mbali vyenye thamani ya Tsh milioni 40 alivyotoa alisema ni pamoja na kitanda cha kujifungulia wajawazito chenye thamani ya Tsh milioni 5.2, darubini, pesa taslimu sh milioni 1, bati zaidi ya 500, rangi debe 20, saruji zaidi ya mifuko 525 na vifaa vingine vingi kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa miradi mbalimbali ya kijiji na ujenzi wa Makanisa, Shule na wodi ya wazazi.

Awali viongozi ukawa wa kijiji cha Mavanga kata kata ya Mavanga walimpingeza mbunge Filikunjombe kwa kuwa mbunge wa mfano Ludewa japo wapo viongozi wengi ndani ya chama chake ni wabovu.

Mwenyekiti wa UKAWA Mavanga, John Mligo akishu

No comments:

Post a Comment