WAWAKILISHI kutoka nchi 75 watashiriki katika awamu ya 32 ya
Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Hayo ni kwa mujibu wa Hujjat-ul-Islam Ahmad Sharafkhani Naibu Mkuu wa Shirika la Awqaf la Iran ambaye ameongeza kuwa mashindano hayo yataanza Ijumaa jioni katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano hapa Tehran.
Awamu ya 32 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yanatazamiwa kuanza katika mji mkuu Tehran mnamo 27 Rajab sawa na Mei 15.
Wasomi (maqarii) na waliohifadhi Qur’ani kikamilifu kutoka nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu watashiriki katika mashindano hayo ya wiki moja.
Mashindano hayo yataanza sanjari na mnasaba wa Mab’ath (kubaathiwa au kupewa utume Mtume Muhammad SAW). Mashindano hayo ya kila mwaka yataendelea kwa muda wa wiki moja hadi Ijumaa
No comments:
Post a Comment