Thursday, May 14, 2015
FAO laonya kutokea la kibinadamu nchini Yemen
SHIRIKA la Kimataifa la Chakula na Kilimo FAO limeonya juu ya kutokea janga la kibinaadamu nchini Yemen.
Kwa mujibu wa shirika hilo, wananchi wa Yemen wanakabiliwa na hali mbaya mno kufuatia kuishiwa na mahitaji muhimu ikiwemo chakula.
Ikiashiria kuwa asilimia 90 ya chakula wanachokipata Wayemen, huagizwa kutoka nje ya nchi, FAO imesema kuwa, uagizwaji huo ulisimama tangu kulipoanza mashambulizi ya Saudia nchini humo. Aidha shirika hilo limeongeza kuwa, kupungua kwa nishati nchini humo ni tatizo jingine lililochangia kuzorota kwa shughuli za ugawaji chakula katika maeneo tofauti ya nchi hiyo. Shirika la Kimataifa la Chakula na Kilimo FAO limeongeza kuwa, hata msaada uliotayarishwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watu wa nchi hiyo, ni mdogo mno usioweza kukidhi mahitaji ya wananchi hao. Limeitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kwa lengo la kuokoa maisha ya raia wa Yemen na kuonya kuwa endapo juhudi za lazima hazitochukuliwa, basi kutashuhudiwa maafa makubwa nchini humo. hayo yanajiri katika hali ambayo jana ndege za utawala wa Aal-Saud, ziliendeleza mashambulizi yake kwa kuyalenga maeneo tofauti ya nchi hiyo na kupelekea makumi ya watu kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment