Saturday, May 9, 2015

PELE afanyiwa upasuaji


PELE wakati akichezea Timu yake ya Brazil
ALIYEKUWA nyota wa timu ya Taifa ya Brazil Abeid  Pele amefanyiwa upasuaji wa kibofu cha mkojo katika hospitali moja mjini Sao Paulo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini Brazil ni kwamba nguli huyo wa mpira wa miguu anaendelea vyema.
Pele mwenye umri wa miaka 74 alilazwa katika hospitali hiyo takriban miezi sita iliopita kwa upasuaji wa dharura ili kuondoa mawe katika figo yake.
Pele ambaye jina lake ni Edson Arantes do Nascimento alifunga zaidi ya mabao 1200 wakati alipokuwa akicheza soka na kuisaidia Brazil kushinda mataji matatu ya kombe la dunia.

No comments:

Post a Comment