Ban Kimon Ktibu mkuu wa Umoja wa Mataifa |
Makundi ya asasi za kiraia yamewaomba raia wa nchi hio kususia kura hio, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akitaka uchaguzi mkuu wa Burundi kuahirishwa.
Makundi ya kutetea haki za
kibinadamu nchini Burundi yametoa wito kwa wapiga kura nchini humo kususia
uchaguzi wa ubunge unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu.
Mashirika hayo yamesema kuwa kwa
sasa mazingira ya kisiasa nchini humo hayawezi kuruhusu uchaguzi huru na wa
haki, kufuatia miezi kadhaa ya ghasia.
Umoja wa mataifa umekuwa ukiendesha
jitihada za kuleta uwiano kabla ya uchaguzi
Makundi hayo ya kijamii yametoa
taarifa ya pamoja yakitoa wito kwa jamii ya Kimataifa kutotambua uhalali wa
uchaguzi huo.
Wakati huo huo katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito kwa utawala wa nchi hiyo kuhairisha uchaguzi
mkuu baada ya vyama vya upinzani kutangaza kuwa havitashiriki.
Makamu wa Rais alitoroka nchini humo
baada ya kumpinga rais Nkurunziza
Takriban zaidi ya watu 50 wameuawa
nchini Burundi tangu mwezi Aprili mwaka huu wakati rais Pierre Nkurunziza
alipotangaza kuwa atawania muhula wa tatu.
Maelfu ya raia wengine wa Burundi
nao wamehamia mataifa jirani kwa hofu ya kuzuka mamchafuko zaidi.
Uchaguzi wa ubunge unatarajiwa siku
ya Jumatatu huku uchaguzi wa urais ukipangiwa kufanyika tarehe 15 Julai mwaka huu.
No comments:
Post a Comment