Wednesday, June 24, 2015

WAPINZANI nchini Misri wahukumiwa jela miaka 15


Wapinzani wa Misri

MAHAKAMA ya kijeshi nchini Misri imewahukumu wapinzani 54 wa serikali ya nchi hiyo, kifungo cha miaka 15 jela.

Gazeti la ash Sharq la nchini Qatar limeripoti kuwa, mahakama ya kijeshi ya Misri leo Jumatano limeendelea kusikiliza kesi ya wapinzani 54 wa serikali ya nchi hiyo waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya kufanya vurugu na kuwahukumu kifungo cha miaka 15 jela kila mmoja wao.
Duru za mahakama za Misri zimesema kuwa, wapinzani 33 wengine wametolewa hatiani na mahakama hiyo.
Watuhumiwa hao ambao wamekimbia nchi, wamehukumiwa adhabu hiyo baada ya kupatikana na hatia ya kushiriki katika maandamano ya wananchi baada ya kupinduliwa na jeshi, Muhammad Morsi, Rais wa zamani wa Misri, maandamano ambayo yaliishia kwenye machafuko.
Maafisa wanne wa polisi na idadi kubwa ya waandamanaji walijeruhiwa kwenye machafuko hayo.

No comments:

Post a Comment