soko kuu la Morogoro |
WANANCHI
wa mtaa wa Kola‘B’kata ya Kichangani Manispaa ya Morogoro wameunda sheria ndogo ya mtaa itakayowaburuza mahakamani
wote watakaokuwa wakuipuuza na kutohudhuria vikao na mikutano inayoitishwa na
serikali yao ya mtaani wakilenga kujenga uwajibikaji na maendeleo ya haraka.
Sambamba na hilo wamezindua dira ya
maendeleo ya mtaa inayoambatana na mpango mkakati wa muda mrefu na mfupi hadi
miaka mitano ijayo.
Akiwahutubia wanachi katika mtaa huo
Mwenyekiti wa mtaa huo Asegelele Mwaitebele alisema lengo la seria hiyo
itakayokwenda sambamba na faini watakayokubaliana sambamba na dira hiyo mtaani
hapo ni kuhakikisha kila mwanachi anashiriki vema katika shuguli za maendeleo
na kubaini haraka walipokosea kasha kurekebisha.
“katika kuandaa mkakati huu tumeunda
kamati za maendeleo zitakazo mshilikisha kila mwanachi kushiriki katika mipango
na shuguli za maendeleo…kuna kamati tisa ikiwemo ya utawala na uongozi pia
kamati ya mipango,fedha na uchumi”alisema Mwaitebele.
Kamati nyingine kwa mujibu wa
Mwaitebele ni Miundombinu na Maji,Maafa,Elimu na michezo,Afya na
Mazingira,ulinzi na usalama,kilimo na ufugaji pia kamati ya Ukimwi na mazingira
hatarishi.
Katika mkutano huo wa kwanza tangu
wachaguliwe Septemba.2014 uliokuwa na agenda sita ikiwemo ya
kutoashukarni,kutambulisha serikali,kamati za maendeleo na mpango mkakati
Mwenyekiti huyo alisema serikali hiyo inakabiliwa na kutokuwa na ofisi pia
vifaa vya kufanyia kazi.
“kulikuwa na sababu kadhaa
zilizotuchelewesha tusiitishe mkutano kubwa ikiwa uongozi ulipita kutotaka
kukabidhi ofisi na ugeni wa kuongoza lakini sasa tumejifua na tupo tayari
kuwaongoza kwa misingi ya sheria na haki”aliongeza.
Awali akimkarisha mwenyekiti huyo
kuzungumza,kaimu mtendaji wa mtaa huo Martin Rumisha mbali kuunga mkono hoja za
mwenyekiti alionyesha kusikitishwa na mahudhurio madogo mkutanoni hapo kisha
kuwataka kutoa wazo la kudhibiti utoro huo.
“mnaweza kutunga sheria ndogo kama
mnavyopendekeza na kuipeleka kwa mkurugenzi wa Manspaa kwa mapitio na
kuidhinishwa kwa matumizi…kumbukeni mikutano hii ni muhimu kwakua inachochea
maendeleo”alifafanua Rumisha.
Aidha kamati ya fedha na uchumi
kuanisha mapema vyanzo vya mapato vinavyoweza kuungizia mtaa huo fedha kwa
maendeleo yake huku akiainisha baadhi yake kikiwemo cha faini ndogo kwenye
makosambalimbali,kufanya harambee na kusaka wahisani yakiwemo mashirika na
taasisi mbalimbali za ndani na nje.
No comments:
Post a Comment