KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha pamoja na mambo mengine kilipitia
mwenendo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo
kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya tathmini ya mwenendo wa timu.
Kamati ya Utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo;
1. Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia Juni 21, 2015.
2. Benchi lote la ufundi la Taifa Stars limevunjwa kuanzia Juni 21, 2015.
3. Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment