Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Peter Pinda |
WAZIRI Mkuu wa
Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda amewaasa watanzania hususani
wanachama wa chama cha mapinduzi CCM nchini kuweka chama mbele.
Akiwashukuru wanachama 45 waliomdhamini katika mbio zake za
kuusaka urais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania jana,Pinda akiwa ameongozana
na mkewe Tunu Pinda katika ofisi za CCM wilaya alisema chama kinauwezo wa
kumtafiti mtu kama anafaa au laa na kuwa kumweka mtu mbele ni hatari kwa amani
ya taifa tuliyonayo.
"kwanza liombeeni taifa liendelee kuwa na manai na utulivu
kwa kupata viongozi wazuri lakini niwausie ninyi wanachama wenzangu na taifa
kwa jumla kuwa tangulizeni mbele msilahi ya chama nasi mtu...msipumbazwe na
uwezo wa mtu na kuwachagua watu wasifaa" alisema Pinda kwa tahadhari na
kuongeza.
Alisema yeye akiwa mjumbe wa kamati kuu ya chama,halmashauri kuu
ya chama na mkutano mkuu angependa kiongozi ajae akijinasibu yeye kuwa na sifa
ya uongozi bora na siyechaguliwa kwa nguvu fulani kama si uwezo wake wa
kusimamia,kuongoza na kutekeleza.
"mpaka sasa bado nakiamini chama kwa sera zake,uwezo wake wa
kuongoza lakini kwa makuzi yake kinafaa kuendelea kuongoza kwa mafanikio
makubwa...kumbukeni kama uaridi halijanichia harufu bali hata uzuri wake maana
nimekuwa kwenye serikali ya awamu ya kwanza katika nyadhifa mbalimbali hadi
leo"aliongeza.
Awali mwenyekiti wa wilaya Fikiri Juma alimweleza pinda kuwa mbali
na mkoa huo kuwa kitovu cha mafanikio yake na kuendelea kuwa kitovu cha
mafanikio ya safari yake alimwahidi kuendelea kumwombea mafanikio ili
watanzania wasipoteze radha aliyoaanza nayo.
No comments:
Post a Comment