CHAMA cha walimu CWT Manispaa ya Morogoro kimewatahadhalisha waalimu
kutoshabikia teknolojia na utandawazi wa kigeni badala yake kimewataka kuwa
wabunifu wa njia za ufundishaji na kuvitambua vipaji vya watoto madarasani
kisha kuviendeleza ili viwe na tija kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Hayo yamesemwa na Katibu wa
chama cha walimu Manspaa ya Morogoro Raphael Maswi kwenye hafla fupi ya
kuwatunuku walimu 10 zawadi ya mifuko 10 ya Saluji kama kifuta jasho kwa kila
mmoja kutokana na utumishi wao kwa jamii akisisitiza ipo hatari ya mila na
desturi zetu kupotea.
Katika hafla hiyo
iliyofanyika katika ofisi za CWT Mkoa,Maswi alisema katika kutambua na
kuthamini mchango wa waimu katika taifa chama hicho Manspaa kimekuwa kikibana
baadhi ya matumizi yake ili kuwezesha walimu hao kuondoka mapumzikoni na kitu
cha kuanzia katika maisha Mapaya.
"mpaka mwezi februari
mwaka huu zaidi ya shilingi 17,380,000 fedha zake za ndani katika ofisi
zimetumika kuwapa motisha wastaafu wanaozidi 60 mwaka 2013/14...tunafanya
hivi angalau kutambua na kuthamini mchango wa mwalimu maana tunaona bado
serikali inasuasua"alifafanua Maswi na kuongeza.
“sio tunaingilia kazi ya
serikali tunataka kuimarisha haiba ya mwalimu,katika mpango huu mwaka 2013
tulitumia shilingi Mil.6 na mwaka 2014 shilingi Mil.4.570 kwa ajili ya samani
na shilingi 6,810,000 kwa ajili ya zawadi”alifafanua Maswi.
Wakiunga mkono juhudi hizo
baadya walimu Monela Mzelu na Frolance Gombe walivitaka vyama vingine vya
wafanyakazi nchini kuiga utaratibu wa chama hichi ikiwemo kutumia fedha kidogo
kuboresha maeneo ya kazi na kutoa mkono wa kwaheri kwa wanachama.
kwa nyakati tofauti
walisena mbali na kada ya elimu kukumbwa na chamgamoto mbalimbali zikiwemo za
maslahi madogo,kutolipwa baadhi ya stahiki na kutelekezwa pindi wanapo staafu
zipo pia kada nyingine ikiwemo Polisi ambazo serikali inapaswa kuitazama kwa
jicho la pili ili kuliendeleza taifa na amani iliyopo.
"unajua amani ndio
kilakitu bila amani hata elimu haitolewi na tunaliombea taifa hili livuke
katika mchakato huu wa kupata viongozi bila hata chembe ya damu kumwagiaka
maana viashiriali vilivyopo ni hatari kwetu wazee na wajukuu zetu"alisema
mwalimu Frolance
No comments:
Post a Comment