Mamlaka ya kukabiliana na majanga ya dharura NDMA imesema kuwa
imepokea maagizo kutoka kwa Nawaz Sharrif kuchukua hatua za dharura.
Jeshi tayari
limepelekwa katika eneo hilo kujenga vituo vya kukabiliana na joto hilo ili
kuisaidia mamlaka hiyo.
Wengi
wa waathiriwa ni watu wazima kutoka kwa familia zinazopata mapato ya chini.
Maafisa wa afya
wanasema vifo vingi vimetokea katika mji mkuu wa Karachi ambao ulikumbwa na
joto la viwango vya juu vya hadi digree 45 c.
Katibu
wa afya katika mkoa wa Sindh Saeed Mangnejo amesema kuwa watu 612 walifariki
katika hospitali kuu ya serikali mji huo katika kipindi cha siku nne
zilizopita.
No comments:
Post a Comment