![]() |
| Balozi Seifu Alli Iddi |
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake, Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Rajabu Rutengwe alisema maadhimisho
hayo yenye kauli mbiu 'watu waliokatika mazingira hatarishi wakati wa dharura'
yanafanyika kwa mara ya pili mkoani hapa hususani wilayani Kilosa kutokana na
wilaya hiyo kukumbwa na majanga ya kibinadamu na mazingira yakiwemo Mafuriko.
"niheshima kubwa kwa mkoa wetu
kufanyika maadhimisho haya kwa mara ya pili ikizingatiwa mwaka 2012 yalifanyika
Manspaa ya Morogoro kwakua ianautangaza mkoa, lakini safari hii yatafanyika
wilayani Kilosa hasa kutokana na wilaya hii kukumbwa sana na majanga ya
kibinadamu na mazingira kama mafuriko"alifafanua Dk Retengwe.
Alisema maadhimisho hayo
yatakayotanguliwa na matukio matatu likiwemo la jana Julai 22 ambapo umoja wa
vijana wa umoja wa Mataifa YUNA kuwakutanisha zaidi ya vijana 200 wenye kati ya
umri wa miaka 15-30 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Tukio lingine ni maonesho na utoaji
huduma kwa jamii ikiwemo uzazi wa mpango,elimu ya huduma ya kwanza katika
majanga na uandikishaji vyeti vya kuzaliwa sambamba na na kutembelea wanachi
majumbani kutoa elimu hiyo kwa siku tatu wilayani kilosa.
Maadhimisho haya yalianza kufanyika
mwaka 1990 ambapo yamekuwa yakiadhimishwa kila 11 Julai ya mwaka ikilenga
kuhamasisha watu kuelewa umuhimu wa takwimu ya watu na Maendeleo na inakadiriwa
karibu watu Mil.60 duniani hususani wanake na watoto katika mwaka 2014 hawakuwa
na makazi kwa majanga

No comments:
Post a Comment