CHAMA cha wataalamu na wakulima wa
mbogamboga nchini (TAHA) kimeombwa kuboresha na kukuza zao la bilinganya ili
kuwawezesha wakulima wa zao hilo kuondoka na umaskini wa kipato.
Ushauri huo
umetolewa hivi karibuni na wakulima wa mbogamboga wilayani Korogwe mkoa wa Tanga wakati wakiongea na Mbiu ya
maendeleo wilayani humo.
Wanapongeza
hatua za kuanzishwa kwa chama hicho nchini kikiwa na lengo la kuwakomboa wakulima
wadogo wadogo, lakini wanapaswa kutambua kuwa wakulimawa mazao ya mbogamboga
wanahitaji msaada wa taaluma sanjari na ule wa masoko.
Wameeleza
kuwa, soko la uhakika na mbinu bora za uzalishaji wa bilinganya inayomudu ushindani wa soko ndiyo
changamoto kubwa kwao

No comments:
Post a Comment