Wednesday, July 15, 2015

POLISI jijini Mwanza linamshikilia mfanyabiashara kwa tuhuma za mauaji


Mkuu wa jeshi la polisi nchi IGP Mangu

JESHI la Polisi mkoa wa Mwanza linamshikilia mfanyabiashara maarufu Jijini humo Juma Mahende, anayemiliki Mabasi ya J4 kwa tuhuma ya kuwapiga risasi watu wawili na kuwapotezea maisha, katika eneo la Boma lililopo kata ya Nyakato Jijini humo.


Ni nyumbani kwa Marehemu Cloud Skalwanda, eneo la Nyasaka kata ya Kiloleli wilayani Ilemela Jijini Mwanza, ambako ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu, wamekutana kuomboleza msiba huo.

Tukio hilo limetokea majira ya saa nne usiku wa kuamkia leo katika eneo la Boma lililopo kata ya Nyakato, baada ya mtuhumiwa Juma Mahende kumuita Marehemu Cloud Skalwanda, na mwenzake Ally Mohamed mkazi wa kata ya Igoma kuzungumza masuala ya kibiashara.

Baada ya tukio hilo nyumbani kwa Marehemu Ally Mohamed kata ya Igoma, simanzi na vilio pia vikatawala, huku chanzo cha mauaji hayo kikielezwa kuwa marehemu hao walikuwa wakimdai mtuhumiwa shilingi milioni 25/=.




No comments:

Post a Comment