Tuesday, November 10, 2015

Dk Shein na Maalim Seif waendelea na mazungumzo

MAZUNGUMZO  ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa visiwani Zanzibar yameendelea huku mkutano uliowaleta pamoja rais Ali Mohammed Shein na kiongozi wa upinzani Seif Sharif Hamad ukifanyika.

Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, mkutano huo wa faragha katika ikulu ya rais ulihudhuriwa na marais wa zamani Ali Hassan Mwinyi na Amani Abeid karume.
Ni mara ya kwanza kwa Dkt Shein ambaye anatoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Bw Seif wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye ni makamu wa rais wa kisiwa hicho kukutana tangu tume ya uchaguzi kufutilia mbali matokeo ya urais.
Kushirikishwa kwa marais hao wa zamani ni thibitisho kwamba kuna harakati za kisiasa zinazoendelea katika juhudi za kukabiliana na tatizo hilo ambalo limezua mgogoro wa kikatiba.






No comments:

Post a Comment