Washangilia wa timu ya Taifa ya Tanzania |
Kenya
imepanda hatua sita hadi nambari 125, nayo Tanzania ikapanda hatua moja na
kutua nambari 135. Taifa Stars walisonga kwenye mechi za kufuzu kwa Kombe la
Dunia 2018 nchini Urusi kwa ushindi wa jumla wa 2-1 dhidi ya Malawi. Malawi wamo nambari 97 kwenye orodha
hiyo.
Ivory
Coast ndiyo inayoongoza barani Afrika katika nambari 22, ikifuatwa na Algeria
iliyo nambari 26 nayo Ghana nambari 30.
Uganda
ndio walio mbele miongoni mwa mataifa ya Afrika Mashariki, wakikwamilia nambari
68 baada ya kupanda hatua saba.
Rwanda
wamo nambari 96 baada ya kushuka hatua tatu nao Burundi nambari 107 baada ya
kupanda hatua sita.
Congo
Brazzaville wamo namba 52, wakifuatwa kwa karibu na DR Congo walio nambari 55.
No comments:
Post a Comment