Monday, January 11, 2016

MACHAFUKO yaendelea nchini Burundi

WATU  watatu wameripotiwa kuuawa katika machafuko yanayoendelea nchini Burundi.

Taarifa zinaeleza kuwa, watu hao wameuawa katika machafuko yaliyoibuka kuanzia Jumamosi na kuendelea jijini Bujumbura baina ya jeshi la polisi na wapinzani wa serikali ya Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa habari, watu wengine kadhaa wamejeruhiwa wakiwamo polisi wawili, huku idadi kadhaa ya wapinzani wengine wakitiwa mbaroni. Wakati huo huo jeshi la polisi jijini Bujumbura limekadhibisha habari ya kuuawa mwandishi wa habari wakati akitekeleza majukumu yake katika machafuko hayo na kusema kuwa, habari hiyo haina ukweli wowote ule.



No comments:

Post a Comment