MFUKO wa elimu, kilimo na Mazingira Ruangwa (MEKIMARU)
umewataka wadau wa mazingira na Kilimo waliopo mikoa ya Mtwara na Lindi kuhakikisha
kuwa matumizi ya dawa za kuulia magugu yanasimamishwa.
Akioangea na wanahabari hivi karibuni jijini
Dar es salaam , Mwenyekiti wa Taasisis hiyo Bwana Issa Mparuka amesema kuwa ,kasi
kubwa ya matumizi ya dawa aina ya weedall hususani katika zao la ufuta wilayani
Ruangwa inatokana na wadau wa kilimo na mazingira kukaa kimya ilihali wanafahamau
madhara yanayosababishwa na dawa hizo .
Amesema kunahitajika elimu kwa wakulima
wa ufuta ili wahame kwenye kilimo hai ambacho ni rafiki wa mazingira.
Wakulima wengi wa ufuta hawatumii njia
za kupalilia badala yake wanatumia madfawa ya kuuuwa magugu.

No comments:
Post a Comment