NAKALA za bajeti rasmi ya serikali ya Nigeria ya
mwaka wa 2016, zimetoweka kutoka bunge la nchi.
kwa mujibu wa mbunge mmoja aliyezungumza na wanahabari
ambaye hakutaka jina lake litajwe.alisema Bunge
la Senate lilishindwa kuanza kujadili mapendekezo ya bajeti hiyo kwa sababu ya
nyaraka hizo kupotea.
Hali hiyo sasa huenda
ikahujumu uchumi wa Taifa hilo ambao umeathirika pakubwa kutokana na kushuka
kwa bei ya mafuta.
Rais
Muhammadu Buhari aliwasilisha nyaraka hizo kwa mabunge yote mawili mwezi
uliopita.
Serikali
ya nchi hiyo ilikuwa imependekeza nyogesa ya asilimia ishirini ya matumizi ya
serikali, na kuifadhili nyongesa hiyo kupitia mikopo zaidi huku bei ya mafuta
ikiendelea kushuka.

No comments:
Post a Comment