Wednesday, January 13, 2016

SERIKALI ya Tanzania yamzawadia ardhi Samatta

Mbwana Samatta
SERIKALI ya Tanzania imemzawadia Ardhi mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa nyumbani Mbwana Samatta  ardhi  kufuatia uhodari wake uliomwezesha kuondoka na tuzo hiyo na kuisaidia TP Mazembe kutwaa kombe la vilabu bingwa Afrika.

Amepewa kipande cha ardhi eneo la Kigamboni, Dar es Salaam na serikali kupitia wizara ya ardhi na nyumba.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na wadau wa michezo nchini Tazania wakiwemo waziri wa michezo Nape Nnauye na Thomas Ulimwengu ambaye ni mchezaji mwenza wa Samatta.


No comments:

Post a Comment