Sunday, March 27, 2016

BENKI ya Dunia kufadhili dola milioni 100 nchini Lebanon

Bodi ya Benki ya Dunia. Mbele, kati, ni Rais wa Benki ya Dunia. Dr. Jim Yong Kim. Picha ya Benki ya Dunia
 Rais wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim, ametangaza leo mkakati mpya wa dola milioni 100, unaolenga kuunga mkono mpango wa serikali ya Lebanon wa kuboresha viwango vya elimu na kuwawezesha watoto wote wa Lebanon na watoto wakimbizi wa Syria kwenda shule kufikia mwishoni mwa mwaka wa shule 2016-17.


Ufadhili huo mpya umewezeshwa na uamuzi usio wa kawaida wa Bodi ya Benki ya Dunia kutoa misingi ya ufadhili iliyotengewa nchi za kipato cha chini pekee, na umefanywa wakati Rais wa Benki ya Dunia akiwa ziarani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon.

Katika makubaliano hayo, ambayo ni sehemu ya Benki ya Dunia kuzisaidia Lebanon na Jordan kufuatia ukarimu wao kwa kuwapa hifadhi wakimbizi wa Syria, fedha hizo zitasaidia kuboresha viwango vya mfumo wa elimu wa Lebanon ambao sasa unakabiliwa na shinikizo kubwa, pamoja na kusaidia katika kupanua upatikanaji wa elimu kwa watoto wote wa Syria wenye umri kati ya miaka mitatu na 18.(Kwas ihsan ya Redio ya UM )








No comments:

Post a Comment