Sunday, March 27, 2016

IRAN iko tayari kuimarisha uhusiano wake na Pakistan

Rais wa Iran Hassan Rouhan 
RAIS  Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Iran iko tayari kuimarisha uhusiano wake na Pakistan katika nyuga zote.


Rais Rouhani amesema hayo mbele ya waandishi wa habari katika siku ya mwisho ya ziara yake nchini Pakistan na kuongeza kuwa, Iran imejiandaa vilivyo kutekeleza vizuri makubaliano yake na Pakistan kama vile kuiuzia gesi nchi hiyo licha ya kuweko vizuizi vingi ikitaraji kuwa Pakistan nayo itatekeleza vilivyo ahadi zake katika suala zima la kumalizia utengenezaji wa bomba la kusafirishia gesi ya Iran kuelekea nchini humo.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekumbushia umuhimu wa bandari ya Chabahar (kusini mashariki mwa Iran) na bandari ya Gwadar (kusini magharibi mwa Pakistan) na kuongeza kuwa, iwapo bandari hizi mbili zitaunganishwa vizuri, basi zitakuwa ni kituo muhimu sana cha kuziunganisha nchi zote za Asia Mashariki kama vile China.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amerejea hapa nchini baada ya kumaliza ziara ya siku mbili nchini Pakistan ambako ameonana na Rais, Waziri Mkuu, mshauri wa Waziri Mkuu katika masuala ya kigeni wa nchi hiyo pamoja na kushiriki katika kikao cha pamoja cha kiuchumi cha wafanyabiashara wa Iran na Pakistan na kuhudhuria sherehe za kutiwa saini hati sita za ushirikiano katika nyuga tofauti.(kwa Ihsan ya Irib )











No comments:

Post a Comment