Monday, March 28, 2016

HELICOPTER yauwa watu 12 nchini Algeria

WATU  wasiopungua 12 wamepoteza maisha Algeria kufuatia ajali ya helikopta wakati ikilinda doria katika eneo la jangwa la Sahara nchini humo.

 Wizara ya Ulinzi ya Algeria imetoa taarifa na kusema helikopta hiyo ilianguka Jumapili kutokana na matatizo ya kiufundi.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa  tukio hilo lilijiri wakati helikopta hiyo ilipokuwa ikiruka baina ya miji ya Adrar na Reggan katika eneo la Tamanrasset.
Uchunguzi umeanzishwa na jeshi la nchi hiyo kuhusu ajali hiyo.
Algeria imekuwa ikipambana na magaidi wa Kitakfiri hasa kundi la kigaidi la Al Qaeda katika eneo la Maghreb AQIM.
Jumapili iliyopita, jeshi la Algeria liliua magaidi wanne na kuwajeruhi wengine watatu katika eneo la jangwani wakati magaidi hao waliposhambulia kituo cha kuzalisha gesi.




No comments:

Post a Comment