Monday, May 30, 2016

DOKTA Bilali awaasa vijana kukabiliana na changamoto za ajira


Makamu wa rais mstaafu Dk Bilali

MAKAMU wa Rais mstaafu, Dk. Mohamed Bilal, amewaasa vijana akiwataka kujenga utamaduni wa kujifunza lugha mbalimbali ili kujijengea mazingira rahisi ya ajira.

Hayo aliyasema   Dar es Salaam juzi kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Lugha na Utamaduni (IFCL).
Alisema   kutokana na kuwapo  changamoto kubwa ya ajira vijana hawana budi kujifunza lugha nyingi za kigeni kwa ajili ya kuwasaidia.
“Ni heshima kubwa kuona kuwa Tanzania imepata fursa kubwa ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho haya ambayo yamejumhisha mataifa 30.

No comments:

Post a Comment