Monday, May 30, 2016

MACHAFUKO chanzo cha serikali ya Msumbiji kufichwa ukweli kuhusu deni


Carlos Agostinho do Rosário

WAZIRI  Mkuu wa Msumbiji amesema kuwa, machafuko nchini humo ndiyo sababu kuu iliyoifanya serikali kuamua kuficha habari kuhusu deni la dola bilioni moja na laki nne la nchi hiyo kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa IMF.

Carlos Agostinho do Rosário ameongeza kuwa, serikali ya Msimbiji imelazimika kuchukua mkopo huo kwa ajili ya kupambana na maharamia na kudhamini usalama wa meli za kibiashara katika fukwe za nchi hiyo. 
Tarehe 20 mwezi huu wa Aprili
Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ulitangaza kuwa, utasimamisha misaada yake ya kifedha kwa Msumbiji kutokana na serikali ya nchi hiyo kutotimiza ahadi zake kwa shirika hilo. Antinette Sayeh mkurugenzi wa idara ya Afrika ya IMF amesisitiza kuwa, mfuko huo hautaipa serikali ya Msumbiji msaada wowote wa kifedha hadi itakapolipa deni la dola bilioni moja kwa chombo hicho. 
Wiki chache zilizopita, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ulikataa kutuma wataalamu wake mjini


No comments:

Post a Comment