BEI
ya sukari Mkoani Morogoro imeendelea
kuwa kitendawili kwa mlaji kutokana na kushindikana kushuka kulingana na bei
elekezi ya serikali iliyotolewa na Waziri Mkuu Majaliwa Kasim aliyoitoa
karibuni kwenye Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania linaloendelea Mjini
Dodoma.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa
habari hizi mkoani Morogoro umebaini bei hiyo inashindikana kushuka kutokana na
bei ya jumla kungangania kwenye bei ya shilingi 96,000 kwa mfuko wa sukari
wenye uzani wa kilo 50.
“unajua ndugu yangu hapa serikali
inajichanganya yenywe,fikiria sukari leo tumenunua mfuko wa kilo 50 shilingi
96,000 yaani kila kilo moja ni shilingi 1,920 hivi ukiuza shilingi 1,800 faida
yako iko wapi ni afadhali waseme tuwe tunagawa bure ndio maana tunauza angalau
shilingi 2000”alisema Kasim Maulidi mfanya biashara wa duka Kihonda.
Alisema serikali inaweza kujipanga
kukabiliana na changamoto ya upungufu wa sukari kwa kuruhusu sukari toka nje
kuingia huku ikirekebisha kodi na ushuru kwenye sukari ya ndani kwani iki jaa
nchini itajirekebisha kulingana na mahitaji na upatikanaji wake kwenye soko.
Pili Ramadhani wa mkazi wa Mji mpya
mjini hapa alisema serikali imeshindwa kurekebisha soko la sukari ikizingatia
kuwa haina uwezo wa kutosheleza mahitaji yay a bidhaa hiyo kwa jamii nakuwa
inapaswa kukaa ikiwakutanisha wataalamu wa biashara na uchumi ili kuifanya bei
ya sukari kusimama katika soko.
Baadhi ya wafanya biashara wa jumla
akiwemo Sadiq Omary na Lucia Kapinga mjini hapa walibainisha kuwa ingawa
serikali imetangaza kuingiza sukari lakini bado wanaipata kwa bei ghali hivyo
kushindwa kumudu bei elekezi ya serikali katika soko la Jumla .
“tunauziwa kwa kati ya shiingi
94,000 hadi 95,500 unadhani mimi nitauza shilingi ngapi wakati na mimi nauza
ili nipate fedha ya kuendeleza biashara na maisha yangu kwa jumla…nadhani
serikali inatakiwa kutulia juu ya suala hili la sukari ili iwe na bei
inayoendana na hali iliyopo”alisema Omary.
Juhudi za kumpata mkuu wa Mkoa
morogoro Dk Kebwe Stephen kuzungumzia changamoto zilizojitokeza hadi bei
kuendelea kubaki juu hazikufanikiwa licha ya kutafutwa mara kadhaa ikiwemo kwa
simu yake ya kiganjani bila mafanikio baada ya simumu yake kuita mara kadhaa
bila kupokelewa.
Hata hivyo mwandishi wa habari hizi
anaendelea kumtafuta kwa ufafanuzi Zaidi juu ya changamoto zilizoj

No comments:
Post a Comment