Wednesday, May 11, 2016

AJUZA wa miaka 72 ajifungua nchini India


Daljinder Kaur

MWANAMKE  wa umri wa miaka 72 amejifungua mtoto mvulana katika hospitali moja nchini India.

Mwanamke huyo alipachikwa mimba kupitia njia ya kitaalamu ya IVF ambapo yai la mwanamke hutolewa kutoka kwenye ovari, kutungishwa mbegu ya kiume na kisha kurejeshwa kwenye mji wa mimba. Yai hilo linaweza kutolewa kwa mwanamke mwingine.
Njia hiyo hutumiwa kuwawezesha wanawake tasa kupata watoto.
Daljinder Kaur alijifungua mtoto wake baada ya kupokea matibabu kwa miaka miwili katika hospitali iliyoko jimbo la Haryana.
Matabibu walifanikiwa kumtungisha mimba kupitia IVF mara yao ya tatu.
Mumewe Kaur ana umri wa miaka 79.(Kwa hisani ya BBC SWAHILI )








No comments:

Post a Comment