WATU
50 wamefariki dunia kwa mafuriko
na maporomoko ya ardhi yaliosababishwa na mvua kubwa katika baadhi ya maeneo
Ethiopia.
Taifa hilo la upembe wa Afrika
linakabiliwa na ukame mbaya kuwahi kushuhudiwa katika miaka 50 huku watu zaidi
ya milioni 10 wakiwa wanahitaji msaada wa dharura wa kibinaadamu.
Ukame huo umezidhishwa kuwa mbaya
kutokana mvua ya El Nino inayoaathiri baadhi ya mataifa Afrika mashariki na
kusini.
Maafisa wa serikali katika wilaya
iliopo kusini mwa Ethiopia Wolaita wamekiambia kituo cha televisheni ya serikali
kuwa watu 41 waliuawa Jumatatu katika maporomoko ya ardhi yaliotokana na mvua
kubwa inayoendelea kunyesha nchini.
Wengine 9 walifariki kuisni mashriki
mwa eneo la Bol ambako mamia ya mifugo pia ilizama.
Maelfu ya watu pia wamepoteza
makaazi yao, walisema maafisa.
Mafuriko yametatiza jitihada za
kuwaisaidia watu wanaohitaji usaidizi baada ya barabara nyingi na vivukio
kuharibika kabisa.
Serikali na mashirika yamisaada
yameanzisha ombi la msaada wa thamani ya dola bilioni 1.4 kuwasiaidia mamilioni
ya watu wanaohitaji kwa dharura chakula.

No comments:
Post a Comment