Monday, May 30, 2016

TAIFA STARS yatoka sare na Harambee star ya Kenya


TIMU ya Taifa ya Tanzania

TIMU ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, jana ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji wao Kenya katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Moi Kasarani, jijini Nairobi.

Mchezo huo ulikuwa wa maandalizi kwa timu zote, kwani zinajiandaa na mechi za makundi kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON), ambapo Taifa Stars inatarajia kumenyana na Misri Juni 4, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa,  Dar es Salaam.
Kikosi cha Taifa Stars kinachonolewa na kocha, Charles Boniface Mkwasa, kiliingia uwanjani bila ya nyota wake wawili wanaocheza soka la kulipwa ambao ni Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji na Thomas Ulimwengu anayekipiga TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Samatta alikua anaitumikia timu yake iliyokua inawania kufuzu kucheza Kombe la Europa wakati Ulimwengu aliumia lakini wote wanatarajiwa kutua nchini Juni 3, mwaka kuikabili Misri.

No comments:

Post a Comment