Saturday, May 21, 2016

WANANCHI Temeke waunga mkono zoezi la usafi kila jumamosi

WANANCHI  wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam walijitokeza katika maeneo mbalimbali ya Mamnispaa hiyo kufanya shughuli za usafi wa mazingira ili kutekeleza agizo la mkuu wa mkoa wa Dar es salaama Bwana Paul Makonda.


Mbiu ya Maendeleo ilitembelea katika kata ya Mbagala kuu manispaa ya Temeke na kuwakukuta wananchi wa eneo la nja ya ngombe wakifanya usafi wa mazingira, huku maduka na maeneo yote ya shughuli za kiuchumi yakiwa yamefungwa .

Wananchi hao wamepongeza hatua ya manispaa hiyo ,kushauri zoezi hilo liwe endelevu na liwe lenye ubunifu zaidi ili kuuleta tifa bna ufanisi stahiki.

Manispaa ya Temeke, jijini Dar es salaa imetoa agizo kwa wakazi wote wa wilaya hiyo kufanya usafi kila siku ya jumamosi.



No comments:

Post a Comment