![]() |
| wachezaji wa timu ya Yanga wakiwa uwanja wa ndege wa Mwl Nyerere |
JIJI la Dar es Salaam jana lilisimama kwa muda, wakati mabingwa wa
Tanzania, Yanga walipowasili wakitokea Angola walikofuzu hatua ya makundi ya
michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF CC).
Mamia ya mashabiki wa Yanga walianza
kumiminika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kuanzia saa tano
asubuhi na hadi kufikia saa nane mchana hali uwanjani hapo ilikuwa si ya
kawaida.
Pia mashabiki wa Yanga
walijipanga barabarani katika maeneo mbalimbali kuanzia Uwanja wa Ndege,
Kipawa, Vingunguti na Tazara, ambapo mara kadhaa msafara wa basi la wachezaji
wa Yanga uliokuwa ukiongozwa na bodaboda kadhaa ulilazimika kusimama mara kwa
mara sababu ya mashabiki walikuwa wanataka kuwaona.
Kivutio kikubwa katika
mapokezi hayo alikuwa kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ aliyepangua penalti ya
dakika ya 90, ambaye mashabiki walikuwa wakimgombea kutaka kumbeba.

No comments:
Post a Comment