MKAPA ateuliwa kuongoza mazungumzo kuhusu mgogoro wa Burundi
Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania Benjamini Mkapa akiwa na Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli
RAIS Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Benjamin Mkapa, ameteuliwa kuongoza mazungumzo kuhusu
mgogoro wa Burundi ikiwa ni jitihada za viongozi wa Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki kataka kuleta amani ya kudumu nchini humo.
Mkapa, aliyeteuliwa na Mkutano wa 17 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki atakuwa kiongozi wa timu ya usuluhishi wa mgogoro wa Burundi katika
kikao kitakachofanyika kuanzia kesho 21 hadi Mei 24 mwaka huu.
Kikao hicho cha usuluhishi kinatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa (AICC) jijini Arusha. Taarifa zilizopatikana zilieleza kwamba pande
zote zinazohusika na mgogoro huo zitashiriki.
Aidha, Mkutano huo wa 17 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki
ulifafanua kuwa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ataendelea kuwa
msuluhishi wa kudumu kutoka jumuiya hiyo.
Serikali ya Burundi ilikubali kufanyika usuluhishi huo na iko tayari kushiriki
katika mazungumzo ya amani yanayofanywa na viongozi wa Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki yakihusisha wadau wote wa siasa nchini Burundi ikiwa ni jitihada za
kuumaliza mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo
No comments:
Post a Comment