Friday, July 22, 2016

ASASI ya mazingira ya CONASU yaanza kurejesha uoto wa asili katika bahari ya Hindi

ASASI ya kutunza mazingira nchini ya
CONASU yenye makao yake makuu mjini Morogoro ikishirikiana na mfuko wa kutunza mazingira duniani ‘World wildlife Fund (WWF)zimeanza kurejesha uoto wa asili ufukweni mwa bahari ya Hindi mashariki mwa Tanzania kwa kupanda mimea maji jamii ya Mikoko pwani ya mji wa Bagamoyo.

Asasi hiyo inayoungwa mkono pia na halmashauri ya mji huo Mkoani Pwani inakusudia kupanda eneo lenye jumla ya ukubwa wa hekta nne ukingoni mwa bahari ya Hindi vikihusishwa vijiji kadhaa kikiwemo cha Mlingotini,Kaole, Kondo na Pande katika kata ya Saadani,Miono,Kange na Mitipini Wilayani Bagamoyo.
Mkurugenzi wa CONASU  Angelus Runji  alisema katika eneo hilo zaidi ya miche 40,000 ya aina mbili za miti hiyo itapandwa ili katika maeneo yaliyoharibiwa na watu kwa shuguli mbalimbali za kijamii ikiwemo upasuaji Mbao, Uchomaji mkaa,ujenzi na sanaa ikiwemo uchongaji vinyago na michezo ya jadi.
“mwaka 2014 tukiwa na mradi wa kupambana na njia haramu za uvuvi na uvuvi endelevu,tulibaini kupungua idadi ya samaki kutokana na mazalia yao ikiwemo Mikoko kufyekwa ovyo hivyo samaki kushindwa kuzaliana kwa urahisi na wengine kupotea kwa kuliwa na samaki wakubwa wengine kufa kwa kushindwa kuishi kwenye kina kirefu cha maji”alifafanua Runji.
Aidha alisema mbali na Mikoko kuwa na umuhimu kwa mazalia ya samaki pia mpango wa baadae ni kuanzisha ufugaji Nyuki katika mikoko hiyo mpango ambao tayari umeanza kutekelezwa kwa baadahi maeneo.
Baadhi viongozi akiwemo mjumbe wa mazingira katika serikali ya kitongoji cha Kitame  Nuru Seif alisema kutoweka kwa mikoko hiyo kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita umewasababishi kuishi maisha duni baada ya kukimbiwa na waume zao wanakwenda mikoa mingine kutafuta.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji hicho cha Kitame Slvester Kangwe mbali na kukili kukutoweka kiwango kikubwa cha Samaki na bahari kushindwa kupumua alibainisha kuwepo ongezeko la kasi ya upepo, gharama ya maisha kupanda huku takribani wakazi 180 wakikimbia kitongoji hicho chenye takribani wakazi 300.

Waliiomba serikali kuwawezesha kwa elimu ya mazingiri,kuwapatia vifaa vya ulinzi,Boti kwa ajili ya ulinzi wa ekari hizo 50 za mikoko,mavazi maalumu ya kuogelea na kuimarisha shuguli za miti hiyo kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo kwa kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wanaohujumu.



No comments:

Post a Comment