JAMII ya walemavu
imejitoa kimasomaso kwa kushiriki kikamilifu shughuli za mazingira kwa kujianda na kupanda miti
takribani ekari thelathini kuanzia mwezi Disemba mwaka huu.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya uchumi na maendeleo ya
walemavu Tanzania (JUMAWATA)Bwana Mshamu Mzanda amebainisha hayo mapema leo
wakati akiongea na wanahabari ofisi kwake jijini Dar es salaam.
Amesema lengo ni kupanda miti ekari hamsini
ifikapo machi 2017 katika shamba lao lililopo Mtamba, wilayani Kisarawe , mkoa
wa Pwani , lakini wataanza na ekari 30 ili kutekeleza sera ya serikalia ya
utunzanji na uhifadhi wa mazingira kwa kupanda miti.

No comments:
Post a Comment