Michezo
rasmi ya ligi hiyo itaanza kupigwa Agosti 20 Kwa Simba SC wakifungua dimba na
Ndanda FC Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, huku Azam wakiikaribisha African Lyon
Uwanja wa Azam Complex,
Chamazi.Kagera Sugar watacheza na Mbeya City Uwanja
wa Kaitaba, Toto Africans watawalika Mwadui FC Uwanja wa CCM Kirumba,Stand
United watakua wenyewe wa wageni wa ligi Mbao FC Uwanja wa Kambarage.
Mtibwa
Sugar watacheza na Ruvu Shooting Uwanja wa Manungu, Turiani, huku Majimaji na
Prisons wakikipiga Uwanja wa Majimaji Songea.Mabingwa watetezi Yanga wataanza
mbio za kuutetea ubingwa wao hapo Agosti 31kwa Kuchuana na Jkt Ruvu katika
dimba la Taifa Dar es Salaam

No comments:
Post a Comment