![]() |
| Wanawake wa kiislamu Nigeria |
Wanawake
hao wameomba shirika moja la kiislamu Hizba linahudumu katika eneo la Kano
lililoko kaskazini mwa Nigeria kuwaunganisha na kugharamia ndoa ya halaiki.
Kamati
maalum ya Hizba ndiyo iliyopewa jukumu hilo la kuwaondolea upweke maelfu ya
wanawake waislamu.
Madhumuni
ya kamati hiyo ya Hizba ni kupunguza idadi ya wanawake waislamu ambao
hawajaolewa.
Hizba
huwakutanisha wanawake na wanaume waislamu kwa lengo la kuwaoza kama
watakubaliana kwa misingi ya dini ya kiislamu.
Wanawake
wengi walimueleza muandishi wetu mjini Kano kuwa wamekuwa wakitafuta waume
wazuri wa kuwaoa lakini hawajabahatika.(BBC SWAHILI)

No comments:
Post a Comment