Wednesday, July 20, 2016

WANAKIJIJI wapinga kauli ya mkuu wa mkoa

Mkuu  wa mkoa wa Morogoro Kebwe Steven Kebwe
WANAKIJIJI Mngazi,Vigolegole na Milengwelengwe kata na tarafa ya Bwakila chini wilayani Morogoro wameandamana kupinga vikali kauli ya mkuu wa mkoa huo wa Morogoro (RC)Dk Stephen Kebwe kuwa wenyeviti wao ndio wanao sababisha migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kuruhusu kiholela uingizaji mofugo katika vijiji hivyo.


Sambamba na hilo wamemtaka mkuu huyo kuwapelekea tafiti zake na vielelezo vinavyobainisha wenyeviti hao kuingiza mifugo katika vijiji hivyo huku wakimtaka Rais Dk John Magufuli kupangua safu ya uongozi mkoa nma wilaya, jeshi la polisi sambamba na kamati za ulinzi na usalama kwa kufanya kazi kwa simu badala ya kwenda eneo husika.

Hata hivyo mkuu wa mkoa huo Dk Stephen Kebwe alisema barua za maelekezo walizotumiwa ni agizo la kitafa katika kushugulikia migogoro hiyo badala yake kuendelea kuwashutumu baadhi ya wenye viti kukaribisha wafugaji vijijini nakuwa tayari imetolewa miezi mitatu kuwatambua wavamizi,idadi ya mifugo na watokako ili uondoshwaji wake uende kwa mujibu wa sheria.
"Barua walizo waonyesha ni maelekezo ya kitaifa kwani katika uondaji mifugo kunataratibu zake kuepusha changamoto nyingine ikiwemo ya magonjwa na maelekezo ya sehemu wanapotakiwa kwenda...vinginevyo itakuwa vurugu isiyo na mwisho"alifafanua Dk Kebwe.
Baadhi yao akiwemo Marium Kibwana,Omary Lukwele na Josephena Magola kwa nyakati tofauti walisema taarifa hiyo ya(RC) kwenye vyombo vya habari imewashitua wakiitafsiri kuwa inalengo la kujiwekea kinga ya kutumbuliwa na Rais kwani tangu viongozi hao akiwemo mkuu huyo wa mkoa wapewe dhamana ya kuongoza hakuna aliyewahi kuoneka katia vijiji hivyo.
 “Walisema wanaamini kuwa mkuu wa mkoa huo ni msomi anyetumia tafiti na vilelezo kutamka jambo hadharani,hivyo kuomba tafiti na vielelezo hivyo ili nawao wamwonyesha vielelezo walivyonavyo dhiidi ya wafugaji hao kuhamia katika vijiji hivyo kisha kulisha mifugo yao kwenye maashamba yao  ya mpunga na mahindi.
“Kama kweli mkuu wa mkoa anauhakika wenyeviti wetu wanaruhusu mifugo kuingia vijijini basi aondoe taratibu alizoweka za kuondosha mifugo kisheria aruhusu vijiji viwaondoe wafugaji hata leo! Alisema Josephna Magala.
Walisema chanzo kikubwa cha ongezeko la mifugo vijijini ni vimemo toka kwa vigogo serikalini na utaratibu mbovu wa kuwafukuza wafugaji unao tegemea kamati za ulinzi na usalama wilaya na mkoa pekee na kuwa utaratibu huo umekuwa hautekelezeki kutokana na viongozi ngazi za juu kupuuza kwa kutofanyia kazi taarifa za viongozi wa vijiji.









No comments:

Post a Comment