Friday, July 29, 2016

WAFANYABIASHARA wa mbogamboga Dar , waomba elimu ya ujasiriliamali na wa mazao

Wafanyabiashara wa mbogamboga 
WANAWAKE  wanaojishughulisha na biashara ndogo ya kuuza mbogamboga  wamewaomba wadau   wa maendeleo hususani katika taaluma ya ujasiriamali na usindikaji wa mazao kuwasaidia kupatia elimu sahihi na yenye tija ya biashara kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.

Baadi ya wananchi wanaouza mbogamboga katika manispaa ya Temek ,jijini Dar  es salaam katika maeneo ya Mtoni mtongani , Mbagala misheni na Mgeni nai wameiambia Mbiu Media kuwa wanashindwa kukabiliana na changamoto ya kudorora kwa bidhaaa zao za mbogamboga kutokana na kukosa elimu sahihi ya ujasiriamali sanjari na ile ya usindikaji na uhifadhi wa mbogamboga katika njia za kisasa.
Wamesema  kuwa, nguvu ya kununua kwa wateja wengi kwa sasa imepungua hali inayochangia mboga nyingi kubaki , hivyo wanahitaji  elimu na ujuzi wa utunzaji na uhifadhi wa mbogamboga hizo pamoja na ujasiriamali.


No comments:

Post a Comment