![]() |
| Mahakama kuu ya Tanzania |
SERIKALI ya Tanzania imewasilisha ombi la
kukata rufaa, uamuzi wa kihistoria nchini uliopinga ndoa za watoto walio chini
ya umri wa miaka 18.
Mwezi uliopita mahakama kuu iliamua kuwa sehemu za sheria ya ndoa mwaka
1971, iliyoruhusu wasichana kuolewa wakiwa na umri wa hata miaka 14 ni kinyume
na katiba.
Kundi la kutetea haki
za watoto "Msichana Initiative" iliwasilisha kesi hiyo mahakamani.
Taarifa hiyo ya kukata rufaa imewashtusha wengi Tanzania , wengi wakishindwa
kuelewa ni kwanini mkuu wa sheria angetaka kugeuza hukumu hiyo.
Mwezi uliopita
mahakama kuu iliipa serikali muda wa mwaka mmoja kurekebisha kosa hilo na
kuweka umri wa miaka 18 kama umri sahihi wa watu kufunga ndoa, kwa wote
wasichana na wavulana nchini.
Awali sheria ya ndoa
ya mwaka 1971 nchini Tanzania imetaja kuwa wavulana wanapaswa kuoa wakiwana
miaka 18 huku wasichana wakiwa na umri wa miaka 15. Kesi hiyo iliwasilishwa na
kundi la kutetea haki za watoto Msichana Initiative, kupitia wakili Jebra
Kambole.
Asilimia 37 ya
wasichana walio na umri wa chini huolewa Tanzania. Wasichana wenye umri wa hata
miaka 14 huozwa kwa idhini ya wazazi. Na wengi wao baadaye huripotiwa
kukabiliwa na unyanyasaji nyumbani na hutengwa katika jamii - wakikosa nafasi
za kusoma na kuajiriwa.
Hivi karibuni bunge
lilikarabati kipengee cha sheria ya elimu na sasa ina sehemu inayotoa hukumu ya
kifungo cha miaka 30 gerezani au faini ya dola 2500 kwa wanaume wanaowapachika
mimba au kuwaoa wasichana wa shule.
(Chanzo BBC Swahili)

No comments:
Post a Comment