![]() |
| Mkulima wa nyanya akiwa shambani |
KUKOSEKANA kwa
viwanda vingi vya kusindika nyanya nchini ni moja ya changamoto itakayowafanya
wananchi wanaojishughulisha na kilimo boiashara kukata tamaa katika sekta ya
kilimo.
Hayo yamebainishwa mapema wiki hii na wakulima wa nyanya
katika kijiji cha Doma, wilayani Mvomero . mkoa wa Morogoro katika mahojiano na
Mbiu Media.
Wamesema kuwa, bei ya nyanya kwa sasa imeshuka na kfikia
tenga moja la debe mbili na nusu kuuzwa shilingi elfu tano kutokana na
uzalishaji wa zao hilo kuongezeka hali inayosababishwa wakulima kutopata faida
stahiki .
Kutokana na na hali hiyo wameiomba serikali ya awamu ya tano
kuhakikisha kuwa inakabiliana na changamoto hiyo ili kumuwezesha mkulima kupambana
na umaskini wa kipato.

No comments:
Post a Comment