Ziwa
Tanganyika ndilo la kale zaidi Afrika na samaki wake huwa muhimu sana kwa lishe
katika mataifa yanayopakana na ziwa hilo.
Lakini
idadi ya samaki imepungua sana, huku wavuvi wakiendelea kuongezeka.
Ongezeko
hili la wavuvi lilidhaniwa kuwa chanzo kikubwa cha kupungua kwa idadi ya
samaki.
Lakini
utafiti mpya unaonesha chanzo hasa ni ongezeko la joto duniani kutokana na
mabadiliko ya tabia nchi.
Ziwa
Tanyanyika ndilo la pili kwa ukubwa duniani miongoni mwa maziwa yenye maji
yasiyo na chumvi na maji yake huwa katika mataifa manne: Burundi, Jamhuri ya
KIdemokrasia ya Congo, Tanzania na Zambia.
Samaki
kutoka kwa ziwa hilo hutoa asilimia 60 ya protini zitokanazo na wanyama ambazo
huliwa na watu eneo hilo.
Aidha,
ni eneo lenye aina nyingi ya wanyama na mimea(bbc SWAHILI)

No comments:
Post a Comment