Friday, August 12, 2016

AFRIKA kusini Kinara wa uchumi barani Afrika


KIONGOZI  wa Nigeria Muhammadu Buhari amelalamika kwamba taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika limekuwa maskini ghafla.

Amesema hayo siku moja tu baada ya Afrika ya kusini kutwaa tena nafasi  ya taifa lenye uchumi mkubwa barani Afrika.
Nigeria ilikuwa imeshikilia nafasi hiyo kwa miaka miwili baada ya kutathmini upya uchumi wake.
Afrika Kusini iliipita Nigeria baada ya kutumiwa kwa viwango vya sasa vya ubadilishanaji wa fedha dhidi ya dola ya Marekani.
Sarafu ya rand ya Afrika Kusini imeimarika pakubwa ilhali naira ya Nigeria imeshuka sana.
Kwa sasa, thamani ya uchumi wa Afrika Kusini ni $301bn (£232bn) nao uchumi wa Nigeria $296bn.





No comments:

Post a Comment