Thursday, September 1, 2016

MDUDU wa nyanya "kantangaze"tishio kwa wakulima

WAKULIMA wa viungo , mboga na   Nyanya  katika kata ya Nyandira wilayani Mvomero, mkoa wa Morogoro  wameitaka serikali kupitia wizara ya Kilimo na chakula,Mifugo na Uvuvi nchini kupitia wanasayansi na watafiti kumtangaza mdudu maarufu Kantangaze ‘Tuta absoluta’janga la kilimo kutokana na kuhatarisha kuteketeza zao hilo nchini.



Hitaji hilo lilitolewa kwa nyakati tofauti na wakulima wa Nyanya Julius Kobero wa Pinde na Christina Kibaga wa Kilangali kwenye warsha ya uhamasishaji njia bora ya kuzalisha mazao hayo kibiashara, tija na masoko iliyoandaliwa na mtandao wa wakulima wadogo MVIWATA ikishirikiana na Gret ya Ufaransa kwa ufadhili wa Jumuia ya Ulaya EU.
“viungo na mbomboga ndio zao letu la uchumi tatizo ni mdudu Kantangaze ukweli anatutia umasikini kwa shambulia na kuharibu mashina,majani na matunda…wanaenea kwa kasi kubwa, seriakali imtangaze janga na itutafutie dawa ya kumwangamiza vinginevyo hatutakuwa na nyanya nchini”alisema Christina.
Walisema endapo serikali itampuuza mdudu huyo ipo hatari kwa wakulima kufilisika na bidhaa hiyo kuwa kosekana nchini kisha kutegemea kutoka nje ya nchi na vyakula vilivyosindekwa jambo ambalo ni hatari kwa afya na kiuchumi kwa watanzania.
Awali wakizungumzia dhamira ya MVIWATA kuwawezesha wakulima hao kuzalisha kwa tija na upatikanaji masoko na uchumi kukua, mratibu wa mradi huo ujulikanao Malimbichi Ernest Likoko na Afisa kilimo wa mradi  Giovanni Nguvu kwa nyakati tofauti walibainisha mdudu huyo kuripotiwa serikalini nakuwa tafiti zinaendelea.
“nikweli ndundu huyo anaweza kutia hasara ya asilimia 100 akiingia kwenye shamba la nyanya kutokana na kasi kubwa aliyoanayo katika kuzaliana ambapo hutaga zidi ya mayai 260 huku na kwa mwaka wanazaliana mara Tisa…sasa mdudu mmoja anataga kiasi hicho fikiria wakiwa 1000 shambani”alisema Nguvu.
Hata hivyo walisema MVIWATA ikishirikiana na wadau mbalimbali ndani na nje wameanza kutumia mitego ya asili kuwanasa wadudu majike wa aina hiyo na juhudi zinaendelea kutafuta njia nyingine kuwakabili wadudu hao ambao ambao wamebainika kutodhulika na sumu zinazotumika katika mazao hayo.
Kupitia mradi Malimbichi wenyelengo la kufikia zaidi ya kaya 16,000 na watu 72,000 mkoani Morogoro, Mviwata inakusudia kuboresha uzalishaji,kupata masoko,ukuzaji uchumi,utunzaji mazao na mazingira ufanyika katika tarafa nne ikiwemo ya Mgeta kata ya Nyandira uzalishaji Nyanya,Matombo(Pilipilimanga,ambalasini na karafuu) na Kilolo kata ya Ruaha mbuyuni(Vitunguu)


No comments:

Post a Comment