Friday, September 9, 2016

MAJI ya mto nchini Urusi yabadilika rangi na kuwa mekundu

WACHUNGUZI  wa masuala ya mazingira nchini Urusi wanajaribu kubaini sababu iliyoyafanya maji ya mto ulio karibu na kiwanda cha nikeli cha kampuni ya Norilsk Nickel kubadilika na kuwa ya rangi nyekundu.

Picha za maji ya mto Daldykan ambayo yamebadilika rangi zimesambazwa sana katika vyombo vya habari Urusi.
Gazeti la serikali la Rossiiskaya Gazeta linasema kuvuja kwa bomba la kusafirisha taka za mchanganyiko wa shaba nyekundu na nikeli huenda likawa kiini cha maji hayo kubadilika rangi.
Norilsk Nickel ndiyo mzalishaji mkubwa zaidi wa nikeli na palladium duniani.(BBC SWAHILI)



No comments:

Post a Comment