Friday, September 9, 2016

TGNP yabuni mbinu za kisasa za kukabiliana na changamoto za umaskini kwa wanawake

MTANDAO wa jinsia nchini TGNP ikishirikiana na asasi ya kimataifa ya Action Aid nchini zimebuni njia mpya ya kupaza sauti za wanyonge kwa kupanda milima ijulikanayo ‘Kilimanjaro’ ambapo leo (Septemba 10) watazindua njia hiyo kwa kupanda milima ya Urugulu Mkoani Morogoro kisha kutamka changamoto zinazoendeleza wimbi la umasikini kwao hususani wanawake vijijini.


Hayo yamebainishwa kwa nyakati tofauti na Mkurugenzi wa TGNP nchini Lilian Liundi na Kaimu meneja wa program na sera Action Aid Elias Mtinda kwenye Tamasha la nne la jinsia ngazi ya wilaya kata ya Mkambarani wilaya ya Morogoro.

“dhamira ya kuwa na Kilimanjaro katika kufikisha ujumbe ni kujenga mfumo mzuri wa kuimkomboa jamii hususani mwanamke kwa kukutoa mawazo na mikakati yake kuanzia ngazi ya familia na wazo hilo kufika ngazi zote za maamuzi kuanzia kitongoji hadi kimataifa” alifafanua Mkurugenzi Lilian.

Alisema lengo la kupeleka maazimio ya wanawake mlima Kilimanjaro hayamaanishi kufanya mapambano na mamlaka zilizopo isipokuwa kuongeza kasi ya jamii iliyoduni hususani ya vijijini kukumbwa kwa uharaka zaidi na kutafutiwa ufumbuzi kupitia njia mbalimbali ikiwemo ya kushirikishwa katika maamuzi.

“lakini pia ikumbukwe kuwa hivi karibuni kutakuwa na mkutano mkuu wan chi za Afrika AU sasa tutamia nafasi hii inayokutanisha viongozi mbalimbali barani Afrika kukutana baadhi ya wanawake kutoka takribani nchi zote barani kuunganisha maazimio yetu na kuyafikisha katika mkutano huo ili ywekwe kama agenda ya kulikwamua bara la afrika”aliongeza Lilian.

Kwa upande wake Kaimu meneja wa Action Aid Elias Mtinda alisema kelelezinazopigwa sasa na wananke dhiidi ya umasini ni zimewezesha jamii kujitambua na kudai pale inapokuwa inahitajika huduma Fulani badala ya awali ambapo jamii ilielemea kuomba ingawa ni haki yao kisheria kutumikiwa.

Akifungua tamasha hilo, mwenyekiti wa Halamashauri ya wilya ya Morogoro Kibena Kingo mbali na kuzipongeza asasi zote ikiwemo TGNP kwa kazi nzuri iliyoamsha ari ya maendeleo wilayani humo aliziomba asasi zote zinazofanya kazi wilayani humo kuwasilisha taarifa katika halamashauri ili kuipa kazi halamashauri kuzikabili changamoto zinazoibuliwa.

“unajua wakati mwingine inakuwa ngumu sana kwa wanachi kutushitaki sisi mbele yao lakini najua kuwa ninyi muwapo huko watasema mengi ambayo sisi tukipata taarifa zake ni rahisi kwa nafasi zetu iwe diwani au mtendeji au hata mkurugenzi na (DC) Mkuu wa wilaya kulitafutia ufumbuzi haraka kabla wanachi hawaja athirika na hayo ndio maendeleo tunayotaka kama viongozi”alifafanua Kibena.

Alisema halmashauri imekuwa ikitumia baadhi ya taarifa za asasi zinazopatikana kupitia njia mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari kutatua kero na changamoto zake hivyo kuzitaka asasi hizo kuwa chachu kwa kufanya hivyo.

Hili ni tamasha la nne la TGNP kufanyika nchini ambapo kwa mara ya kwanza lilifanyika Kisarawe mwaka 2010,Mkambarabarani (2012), Tarime Mkoani Mara(2014) na linarudiwa tena Mkambarani mwaka huu likibebe mada kuu ya ardhi na mwanamke.




No comments:

Post a Comment