![]() |
| Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Steven Kebwe |
DIWANI kata ya Mbuyuni Manispaa ya Morogoro amemwangukia mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Steven Kebwe akimwomba kumwongezea nguvu ya uharakishwaji utatuzi wa
changamoto zinazo wakabili katani humo ikiwemo ya upungufu vyumba vya
madarasa,kukosefu wa maji na matundu ya vyoo shule ya msingi Mbuyuni.
Mbele ya Mkuu huyo wa
Mkoa wa Morogoro Dk.Kebwe na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro,John
Mgalula wakati jumuiya ya Bohora mkoani Morogoro wakikabidhi madawati
50 shuleni hapo, Diwani Msuya alisema sambamba na tatizo hilo kuisha bado
kunachangamoto zinazo fifisha elimu.
Diwani huyo alisema
tangu shule hiyo ianzishwe mwaka 1969 inakabiliwa na changamoto ya miundombinu
mibovu kutokana na jamii wakiwemo wazazi kutokuwa na ari ya kujitolea kuboresha
elimu na kusisitiza juhudi za kipekee zinahitajika toka serikalini kufanikisha
lengo.
Afisa mtendaji wa Kata
hiyo,Jeniffer Rashid katika taarifa yake kwa mkuu huyo shuleni hapo akifafanua
baadhi ya mapungufu kuwaa ni kupungua nyumba za walimu 25,matundu ya
vyoo17,maktaba,chumba cha ushauri nasaha,meza 18, viti 20 vya walimu na kabati
9.
Shule ya msingi Mbuyuni
inawanafunzi 7322 huku ati yao 6771 wakiwa ni watoto wa awali walioandishwa
mwaka huu na 551 wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi darasa la saba.

No comments:
Post a Comment