Monday, March 31, 2014

Walemavu watembea kilomita saba kufuata huduma ya maji.JAMII ya walemavu wasishio kijiji cha Mtamba ,kata ya Kibuta wilayani Kisarawe wanatembea umbali wa kilomita saba kufuata huduma ya maji kutokana na eneo kijiji hicho kukosa huduma hiyo muhimu kwa maisha ya mwanadamu.John Obedi ambaye ni katibu mkuu wa JUMAWATA ameyaeleza hivi karibuni wakati akiongea na wanahabari katika ofisi za JUMAWATA zilizopo Ilala jijini Dar es salaam.Katibu huyo amesema kuwa, gharama za kununua maji kijiji cha walemavu cha Mtamba ni kubwa na walemavu hawana kipato cha kuwawezesha kuweza kumudu gharama hizo,kwani dumu moja la lita ishirini linauzwa kwa shilingi 800 na wastani matumizi ya maji kwa siku kwa famili moja ni dumu tano za lita ishirini ambayo yanahitaji uwe na shilingi elfu nne.KUTOKANA na hali hiyo wamewahimiza na kuwaomba wada na wapenda maendeleo nchini kuwasaidia kutatua kero hiyo ya maji kijijini hapo kwani kama hali hiyo itaendelea kuna uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya kuharisha , kutapika na kuhara damu.

No comments:

Post a Comment