Thursday, April 17, 2014

JESHI la polisi mkoani Iringa la kusanya shilingi milioni 307



JUMLA ya shilingi million 307 zimekusanywa na jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani mkoani Iringa kufuatia   makosa 10,243 katika kipindi cha miezi mitatu ya Januari  hadi Machi  mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini  kwake leo kamanda wa polisi kitengo cha usalama barabarani mkoani humo,B wana Leopord Fungu amesema idadi ya makosa ya usalama barabarani yameongezeka kutokana na maderava wengi kutofuata sheria  na kusababisha kulipishwa faini.

Bwana Fungu amesema makosa hayo yameongezeka ukilinganisha na kipindi kama hicho kwa mwaka 2013 kutoka makosa 61,52 hadi makosa 10,243 kwa  mwaka huu.

Alisema katika kipindi cha Januari 1 hadi Machi 31 mwaka 2013  jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kilikusanya jumla ya shilingi milioni 185.8 likiwa ongezeko la shilingi milioni 121.4 kwa kipindi hicho kwa mwaka huu.

Kamanda Fungu ameyataja baadhi ya makosa hayo kuwa ni makosa ya mwendo kasi , ubovu wa magari, kutofuata ratiba, kuzidisha abiria, matumizi mabovu ya barabara,kutofunga mikanda,kubeba mizigo isiyoruhusiwa kisheria,kutovaa helment pamoja na kupakiza abiria zaidi ya mmoja kwa waendesha pikipiki

No comments:

Post a Comment