Thursday, April 17, 2014

ZAIDI ya watanzania milioni 27 wana simu kadi



IMEELEZWA kuwa zaidi watanzania milioni ishirini na saba wana simu kadi  huku watumiaji wa huduma ya mtandao (internet)wakiwa milioni tisa nchi nzima.

 Hayo yamebainishwa mapema leo na Naibu  mkurugenzi wa masuala ya watumiaji wa huduma za mawasiliano toka Tume ya mawasiliano nchini (TCRA)Bwana Isaack Mruma wakati akitoa ufafanuzi kwa waziri wa nchi  ofisi ya Raisi  uratibu na mahusiano  Mheshimiwa Steven Wasira wakati akikagua mabanda ya Taasisi na idara mbalimbali za serikali kwenye maonesho ya Muungano yanaendelea mnazi mmoja jijini Dar es salaam.

Kuhusiana na madai yanayotolewa na watu wengi kuwa amatumizi ya simu za mkononi yana madhara  kwa watumiaji , Bwana Mruma ameeleza kuwa, mpaka sasa haijathibitishwa kitaaluma na madai hayo si sahihi kwani   Taasisi ya afya Duniani (WHO)imekanusha madai hayo na kusisitiza kuwa hakuna madhara ya kutumia simu za mkononi sanjari  na kuishi jirani na minara ya simu .




No comments:

Post a Comment