TUME ya Taifa ya kudhibiti ukimwi nchini
(TACAIDS) imeweka mkakati wa tatu wa miaka mitano wa kuhakikisha
vifo vitokanavyo na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi vinapungua na
kufikia sifuri ifikapo mwaka 2018.
Afisa
sera na mipango kutoka Tume hiyo Bwana Richard Ngurwa ameyasema hayo
jana mjini Morogoro wakati akizungumza na wadau kuhusu utekelezaji wa mpango
mkakati wa tatu wa Taifa wa miaka mitano wa kudhibiti ukimwi ambapo amesema
pamoja na maambukizi kushuka kutoka asilimia 7.0 hadi kufikia 5.3, bado ipo
haja kwa TACAIDS kufikia malengo kwa kuwa na programu maalumu
zitakazowawezesha watumishi wa afya kupanga bajeti na kufanikisha malengo hayo.
Akichangia katika semina hiyo , kaimu katibu Tawala mkoa wa
Morogoro Bwana Noel Kazimoto amesema jukumu la kuzuia maambukizi mapya ya
virusi vya ukimwi ni la kila raia wa Tanzania bila kujali jinsia,huku mratibu
wa TACAIDS mkoa wa Morogoro Nyangusi Laiza,akiwasisitiza wadau kuupa
kipaumbele mkakati huo ili kufikia malengo ya Tume hiyo kama yalivyokusudiwa
No comments:
Post a Comment